Fahamu njia rahisi za kunywa maji

HomeElimu

Fahamu njia rahisi za kunywa maji

Njia moja wapo ya kutunza afya yako ni kwa kunywa maji kwani husaidia kumeng’enya chakula pamoja na kupunguza uzito wa mwili. Lakini katika kufanya hivyo kuna njia sahihi za kunywa maji nazo ni,

Tumia gilasi au kikombe 

Hakikisha unatumia gilasi au kikombe kwani itakua rahisi wewe kuweza kumaliza maji yaliyomo tofauti na unywapo kwa kutumia chupa.

kaa , epuka kusimama

Kunywa maji wakati mwili wako umetulia na ukiwa umeketi, hii itasaidia maji kwenda kwenye sehemu husika tofauti na unywapo ukiwa umesimama.

Kunywa taratibu

Usinywe maji kama unakimbia au una haraka, hakikisha umetulia ndipo unywe ili kuepuka kupaliwa.

error: Content is protected !!