Jay Z rasmi Instagram

HomeBurudani

Jay Z rasmi Instagram

Msanii wa Hip Hop wa kwanza kuwa bilionea, mfanyabiashara Shawn Corey Carter maarufu kama Jay Z amejiunga rasmi kwenye mtandao wa Instagram na kufanikiwa kupata wafuatiliaji (followers) milioni 1.1 na kupata uthibitisho wa ‘blue tick’ ndani ya masaa matatu tangu ajiunge huku akiwa amemfollow mtu mmoja tu ambaye ni mke wake Beyonce.

Jay Z ameweka picha moja ya filamu ya ‘The Harder the Fall” iliyoachiwa mwezi OKtoba 22 mwaka huu itakayoanza kuonyeshwa kwenye mtandao wa Netflix Novemba 3 mwaka 2021, hukundani ya masaa machache imepata maoni elfu 19 na kupendwa (likes) na watu 295,297.

Beyonce ambaye hakuwa amemfollow mtu yoyote kwa sasa ameamua kumfollow mume wake tu kwenye ukurasa wake wa Instagram.

error: Content is protected !!