Alawiti na kubaka kisa chumvi

HomeKitaifa

Alawiti na kubaka kisa chumvi

Jeshi la polisi mkoani Geita linamtafuta mkazi wa kijiji cha Bukori (jina limehifadhiwa), kwa tuhuma za kuwabaka na kuwalawiti watoto watatu wa darasa la tatu wa familia moja wa Shule ya Msingi Bukori waliogunduliwa baada ya kushindwa kupata haja kutokana na sehemu zao za siri kuumizwa na kuharibika.

Henry Mwaibambe, Kamanda wa Oilisi Mkoa wa Geita alisema kuwa tukio hilo limetokea katika Kijiji cha Bukori wilayani Geita na kueleza kuwa uchunguzi wa awali ulibaini kuwa mtuhumiwa huyo ni mwanafamilia.

“Ukatili mbaya sana upo ndani ya familia, kuna kesi pale Bukori upepelezi bado unaendelea,ndani ya familia kuna mtu mfanyabiashara sijui yuko wapi, kila akija anawaingilia watoto na kuwaambia wasiseme na kwenye familia hiyo mtuhumiwa huyo yeye ndiye mwenye uwezo wa kifedha anawapatia fedha za chumvi,” alisema na kuongez:

“Kuna watoto watatu anawafanyia ukatilii wa kingono, siku ya kugundulika kwa tukio hilo mwanafunzi mmoja aliingia chooni kujisaidia katika Shule ya Msingi Bukori akashindwa kutokana kwa kuwa sehemu ya haja kubwa ilikuwa imeharibika na wanafunzi wenzake walikuwa wakipiga kelele mbona hautoki chooni ili wengine waingie, hadi mwalimu alipofika akaingia akakuta mwanafunzi huyo akiwa kwenye maumivu makali,” alisema Kamanda Mwaibambe.

Aidha, Kamanda Mwaibambe aliwatahadharisha wananchi wa mkoa huo kuwa wamebaini usafiri wa bajaji ni hatarishi kwa kuwa kuna matukio ya ukatilii wa kijisnia na uhalifu mwingine.

error: Content is protected !!