Harmonize: sifanyi promotion

HomeBurudani

Harmonize: sifanyi promotion

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Rajab Abdul maarufu kama Harmonize, amekanusha taarifa za kuwepo kwa video ya nyimbo yake kama baadhi ya waandishi wa habari walivyokua wakiripoti.

Taarifa hizo zilitokana na bango ambalo limewekwa barabarani maeneo ya Kinondoni Manyanya linalomuonyesha Harmonize akiwa na aliyewahi kuwa mpenzi wake, Kajala Masanja likiwa limeandikwa “Lovers” hivyo waandishi na mashabiki wa msanii huyo wakihisi kuwa  ni sehemu ya tangazo la nyimbo yake.

Kupitia Insta Story Harmonize amesema hayo yanayoendelea sio sehemu ya kupiga debe “promotion”  kazi zake bali ni mambo binafsi yanayogusa maisha yake. Pamoja na hayo Harmonize aliomba asiingiliwe na mtu yoyote kuhusu mambo yake hayo binafsi.

Ujumbe mwingine ulioonekana ni Harmonize akimuomba msamaha kwa mtu ambaye hajamtaja jina ila amemwandika kama binti yake unaosema anatamani kuiona familia yake pamoja kwani ameikumbuka.

Ikumbukwe mwanamzuki huyo alishawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi ya muigizaji Kajala Masanja ambapo wawili hawa hawakudumu muda mrefu, Mahusiano ya wawili hawa yalivunjika huku ikidaiwa kuwa harmonize alijaribu kumtongoza mtoto wa Kajala anaejulikana kama Paula Kajala.

Baada ya kuvunjika kwa mahusiano hayo Harmonize alianza mahusiano mapya na mwanadada mwenye asili ya Australia anaejulikana kama Briana.

error: Content is protected !!