Fahamu mambo haya 3 kabla hujamvisha pete

HomeElimu

Fahamu mambo haya 3 kabla hujamvisha pete

Kumvesha pete mwanamke unayempenda na kujua kwamba atakufaa katika safari yako ya maisha sio jambo baya bali kuna vitu unapaswa kuzingatia kabla ya kufikia hatua hiyo, hasa kama unataka kumvesha pete hadharani yani mbele za watu.

Kabla hujachukua hatua ya kuvalisha pete ya uchumba mwanamke wako hakikisha unazingatia mambo haya matatu,

Ni mtu mwenye aibu?

Siku zote watu wenye aibu hawapendi mambo yao yawekwe hadharani na endapo utamvesha pete kwenye hadhara ya watu utamfanya aseme ndio kwa kuhofia kusemwa na watu lakini moyoni hajakubaliana na wewe.

Wote mmekubaliana kuingia kwenye ndoa?

Usifanye maamuzi haya kumvalisha pete ya uchumba mwanamke wako bila kujua kama nayeye yupo tayari kwa muda huo au bado.

Hakikisha una muuliza au ufanye uchunguzi kujua mawazo yake yapoje ili usije ukajuta baadaye na pia ni vizuri mkazungumza suala hili kabla yakulitenda.

Mchunguze angependa avalishwe wapi na vipi pete

Ili uweze kumfanya awe na furaha zaidi hakikisha umemchunguza na kujua angependa siku yakuvishwa pete iweje, sehemu gani na hata aina ya watu ambao angependa wawepo siku hiyo.

error: Content is protected !!