Monalisa asimulia kilichomkuta Sonia

HomeBurudani

Monalisa asimulia kilichomkuta Sonia

Msanii wa filamu, Yvonne Cherrie maarufu kama Monalisa ameeleza maisha yake yaliyokuwa baada ya binti yake, Sonia kukwama Ukraine kwa sababu ya vita vilivyotokana na Russia kuivamia na kushambulia nchi hiyo.

“Kama mzazi maisha yalikuwa magumu kiasi cha kuathiri mambo yote niliyokuwa nikifanya, ikiwamo kazi, kushindwa kula na kutokana na kukosa hamu ya kula nimeoungua uzito wa mwili kilo nane mzima.

“Kiukweli nilikuwa nikiishi kwa mawazo sana, chakula wala sikutamani,nadhani hii ndio moja ya vitu vilivyochangia kunipunguza hata uzito wangu, kwani awali kabla ya sakata hili la vita nilikuwa nina kilo 76 na sasa ninazo 68,” alisema Monalisa.

Kutokana na hali hiyo Monalisa ameamua kumruhusu Sonia apumzike nchini Hungary huku akitafakari atakapo kwenda kusoma tena.

“Amepitia mambo mengi akiwa na umri mdogo, nimekubaliana naye acha abaki nchini Hungary apumzishe akili, kuliko kuanza msukosuko wa kurudi nyumbani, atulie kwanza.

“Mapema mno kujua ninataka Sonia asome nje au hapa nchini, najipa muda kwanza maana nilikuwa ninawaza mambo mengi moyoni mwangu wakati binti yangu akiwa katika ardhi yenye vita inayotumia silaha kali yakiwamo makombora,” alisema Monalisa.

 

CHANZO: MWANANCHI

error: Content is protected !!