Diamond afanya kufuru

HomeBurudani

Diamond afanya kufuru

Mkurugenzi Mkuu wa Wasafi Media na mwanamuziki wa bongo fleva, Naseeb Abdul maarufu kwa jina la Diamond Platnumz amefanya kufuru kwenye sherehe ya harusi ya mmoja wa wafanyakazi wa Wasafi Redio, Diva kwa kumpatia zawadi lukuki zenye thamani kubwa.

Akizungumza usiku wa jana Machi 25, 2022 kwenye Ukumbi wa Hyatt Regence Hotel sehemu ilipofanyikia sherehe hiyo alitoa zawadi ya kiwanja maeneo ya kigamboni, simu mbili za itel, televisheni 2, ameahidi kumpeleka soda aina ya Pepsi nyumbani kwao kila mwezi na kumpa fedha shilingi milioni 10 na kusema kuwa hizo ni shukurani kutoka kwake kwenda kwa Diva kwa kufanyakazi vizuri tangu amejiunga na Wasafi.

Watu wengine maarufu waliotoa  zawadi ni pamoja na Msanii Zuchu ambaye alitoa pesa.

Na Mkuregenzi na Mmiliki wa Zamaradi Tv, Zamaradi Mketema pia alitoa zawadi lukuki kwa Diva.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Zamaradi Mketema (@zamaradimketema)

error: Content is protected !!