Majibu ya Mbwana Samatta baada ya Taifa Stars kufungwa

HomeMichezo

Majibu ya Mbwana Samatta baada ya Taifa Stars kufungwa

Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Mbwana Samatta amesema kuwa wapinzani wao timu ya Taifa Benin, walikuwa vizuri kwenye ulinzi ndio sababu walishindwa kupenya na kufunga goli/magoli.

Samata amesema hayo akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo huo wa kuwani kufuzu Kombe la Dunia nchini Qatar mwaka 2022 uliopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Licha ya kipigo hicho cha goli 1-0, Samatta amesema kwamba hawajakata tamaa na kwamba wanakwenda kupambana katika mchezo wa marudiano nchini Benin kwani wanatambua umuhimu wa kushinda mchezo huo.

Mashabiki wameeleza kuchukizwa na matokeo hayo, hasa nafasi zilizopotezwa na wachezaji Simon Msuva, Kibu Denis na John Bocco ambao wamesema walishindwa kuwa makini na kutumia nafasi za wazi walizopata kwenye mchezo huo.

Kufuatia matokeo hayo, Tanzania imeshuka hadi nafasi ya Tatu kwenye msimamo wa Kundi J ikiwa na alama 4 baada ya michezo mitatu ambapo imeshinda mmoja, kutoka sare mmoja na kupoteza mmoja.

DR Congo ndiyo inayoongoza kundi ikiwa na alama saba, ikifuatiwa na Benin ikiwa na alama tano huku Madagascar ikiwa haina alama.

Tanzania itarudiana na Benin Oktoba 10 mwaka huu, na michezo mingine itarudiana na DR Congo Novemba 11 na dhidi ya Madagascar Novemba 14.

error: Content is protected !!