UTAFITI TWAWEZA : Fursa nyingi za ajira zinapatikana vijijini

HomeKimataifa

UTAFITI TWAWEZA : Fursa nyingi za ajira zinapatikana vijijini

Taasisi isiyo ya kiserikali ya TWAWEZA imesema utafiti uliofanyika hivi karibuni kwa njia ya simu ambapo jopo la wahojiwa 3,000 waliopigiwa simu umeonyesha kwamba asilimia 73 ya wananchi wa vijini wana fursa za kupata ajira kuliko wale wa mijini.

Kupitia utafiti huo TWAWEZA waliuliza swali la “Kwa maoni yako, ni matatizo gani makubwa yanayoikabili kaya yako kwa sasa?, asilimia 27 ya watu kutoka vijijini walisema kukosa ajira na hivyo 73% hawakuona kama ni tatizo hivyo kuthibitisha kwamba vijijini kuna fursa.

Utafiti uliofanywa na TWAWEZA

Hivi karibuni tumeona namna ambavyo serikali inavyofanya juhudi za kuhakikisha inaboresha huduma vijijini na kutengeneza fursa za ajira hasa kupitia kilimo kwani ndio uti wa mgongo wa taifa letu.

Rais Samia Suluhu amewezesha ndani ya muda mfupi kupatikana kwa bajeti bora ya kilimo ambapo kwa mwaka huu wa fedha 2022/23 Wizara ya Kilimo imetengewa Sh Bilioni 751 huku Sh bilioni 631 zikielekezwa kwenye miradi ya maendeleo.

Kuhakikisha fursa zaidi zinapatikana vijijini, serikali ya awamu ya sita kupitia wakala wa usambazaji umeme vijijini (REA) wametenga bilioni 2 kwa ajili ya kukopesha wajasiriamali wadogo wanaotaka kujenga vituo vya mafuta vijijini.

Serikali imetambua kwamba hakuna maendeleo ya viwanda bila malighafi, hakuna chakula bila kilomo, hakuna afya bora bila kilimo, hakuna mapato bila kilimo na hakuna dunia bila kilimo na ndio maana imewekeza kwenye kilimo na kusihi wananchi hasa vijana kujishughulisha na kilimo kwani fursa zipo nyingi.

error: Content is protected !!