Fahamu kuhusu hali ya Uviko-19 duniani

HomeKimataifa

Fahamu kuhusu hali ya Uviko-19 duniani

 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dk. Tedros Ghebreyesus amesema watu hawapaswi kujisahau wala kuchukulia kama janga la Uviko-19 limeisha kwa sababu linaendelea kuua mamilioni ya watu duniani.

Dk Tedros aliyekuwa akizungumza na waandishi wa Habari jijini Geneva Uswisi, Agosti 25 mwaka huu amesema “hatuwezi kusema tunajifunza kuishi na Uviko-19 wakati watu milioni 1 wamekufa na Uviko-19 mwaka huu pekee.”

Amewaambia waandishi wa habari kuwa miaka miwili na nusu ya janga la Uviko-19 duniani “tuna nyenzo zote tunazohitaji za kuzuia vifo vitokanavyo na janga hili.”

Amezitaka serikali zote ulimwenguni kuimarisha juhudi zao za kutoa chanjo kwa wahudumu wote wa afya, wazee, na wengine walio katika hatari kubwa zaidi, mbinu hii ikiwa ni moja katika njia za kuweza kufikia utoaji wa chanjo ya Uviko-19 kwa asilimia 70 kwa watu wote ifikapo Desemba 2022.

“Inafurahisha kuona kwamba baadhi ya nchi zilizokuwa na viwango vya chini zaidi vya chanjo sasa zinainuka hususan barani Afrika,” amesema.

“Inafurahisha sana kuona kwamba utoaji chanjo unazingatia makundi yanayohitajika kupewa kipaumbele huku nchi nyingi zikipiga hatua ya kuvutia katika kutoa chanjo kwa asilimia 100 ya wafanyakazi wa afya na asilimia 100 ya wazee.”

Hata hivyo Dk Tedros amesema bado mengi zaidi yanahitajika kufanywa ili kutokomeza janga hilo la Afya ulimwenguni.

error: Content is protected !!