Matokeo Kidato cha Nne 2023

HomeKitaifa

Matokeo Kidato cha Nne 2023

Baraza la Mitihani (NECTA) limetangaza watahiniwa 484,823 sawa na 87.65% wa mtihani wa kidato cha nne uliofanyika Novemba 2023 wamefaulu.

Akitangaza matokeo hayo leo Januari 25, 2024, Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Dk Said Ally Mohamed amesema kati ya watahiniwa hao wasichana waliofaulu ni 257,892 sawa na 86.17% wakati Wavulana waliofaulu ni 226,931 sawa na 89.40%.

Amesema mwaka 2022 waliofaulu walikuwa ni 476,450 sawa na 86.78%, hivyo ufaulu wa watahiniwa umeongezeka kwa 0.87% ikilinganishwa na mwaka 2022.

“Kati ya Wanafunzi hao waliofaulu kuna watahiniwa wa shule na watahiniwa wa kujitegemea ambapo jumla ya watahiniwa wa Shule 471,427 kati ya 527,576 wenye matokeo ambao ni sawa na 89.36% wamefaulu ambapo wamepata madaraja ya I, II, III na IV,”

“Mwaka 2022 watahiniwa waliofaulu walikuwa 456,975 sawa na 87.79% hivyo ufaulu umeongezeka kwa 1.57%“ “watahiniwa wa kujitegemea waliofaulu mtihani ni 13,396 sawa na 52.44%, mwaka 2022 watahiniwa wa kujitegemea 19,475 sawa na 68.34% walifaulu mtihani huo, hivyo ufaulu wa Watahiniwa hao wa kujitegemea umeshuka kwa 15.90% ulinganisha na mwaka 2022.” Amesema.

error: Content is protected !!