Lusinde: Zitto aombe radhi

HomeKitaifa

Lusinde: Zitto aombe radhi

Mbunge wa Mvumi, Livingstone Lusinde maarufu kama kibajaj amemtaka Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe kuomba radhi kwa madai ya kumsema vibaya Hayati John Mafuguli.

Lusinde ameyasema hayo Bungeni Dodoma baada ya kauli ya Zitto Kabwe ya kusema wanaompenda Magufuli wakazikwe naye.

“Kusema wanaompenda Magufuli wakazikwe na Magufuli maana yake nini? Hii ni kashfa kubwa sana Zitto aombe radhi asirudie tena,

“Tusifikiri kumsema vibaya Magufuli kutasaidia, hawezi kujibu. Hayupo, kama una tatizo naye maliza utakuja kukutana naye kwa Mungu. Mtu akishatangulia kitabu chake kinafungwa, tunamuachia Mungu kuja kutoa hukumu, “ amesema Mbunge wa Mvumi, Livingstone Lusinde.

Mbunge Lusinde pia amesisitiza kwamba Kiongozi huyo wa ACT-Wazalendo anapaswa kuomba radhi kwa Watanzania kwa kumsema vibaya Hayati Magufuli. 

 

error: Content is protected !!