Wahitimu kukopeshwa kwa vyeti vyao

HomeKitaifa

Wahitimu kukopeshwa kwa vyeti vyao

Serikali imesema inaangalia uwezekano wa kutumia vyeti vya wahitimu wa vyuo vikuu nchini kama dhamana ya kuwapa mikopo mbalimbali ya kuwawezesha kujiajiri na kuajiri wengine.

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayamsi na Teknolojia, Omari Kipanga jana bungeni akijibu swali ya nyongeza la Mbunge wa Mlalo, Rashid Shangazi, akibainisha kuwa serikali ina mifuko zaidi ya 45 inayohusika na mikopo mbali na mikopo itokanayo na asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri inayotolewa kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.

“Tunaanagalia namna gani wahitimu watatumia vyeti vyao kupata mikopo tutaifanya tathmini na kufanya uamuzi, hili ni jambo mtambuka, linahusu wizara nyingine. Tunachukua ushauri ili tuone kama vyeti vinaweza kutumika kumdhamini mhitimu,” alisema Kipanga.

Aidha, Naibu Waziri Kipanga alisema halmashauri zinatenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vijana, asilimia nne wananwake na asilimia mbili kwa watu wenye ulemavu.

 

error: Content is protected !!