Mtwara wang’oa vibao vya anuani za makazi

HomeKitaifa

Mtwara wang’oa vibao vya anuani za makazi

Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani imeeleza kusikitishwa na vitendo vya baadhi ya wananchi vya kung’oa vibao vya anuani ya makazi.

Kufuatia tukuio hilo, Halmashauri ikishirikiana na vyombo vya dola inatarajia kuanzisha msako mkali kwa ajili ya kuwakamata watakaohusika katika vitendo hivyo.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara- Mikindani, Kanali Emmanuel Mwaigobeko, amesema halmashauri inawaomba wananchi kuwa walinzi na kutoa taarifa kwa vyombo vya sheria kuhusu wanaojihusisha na ung’oaji wa vibao hivyo.

“Tunatarajia kufanya msako ili kuwabaini na kuwachukulia hatua watakao bainika kujihusisha na ung’oaji wa vibao vya anuani na makazi na kuwachukulia hatua za kisheria, ikiwa ni pamoja na kurejesha gharama zote ambazo zilihusika kuweka hizo anuani,” alisema Kanali Mwaigobeko. 

Mweyekiti wa mtaa wa mtepwezi Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara, Mbuta amekiri kuwepo kwa wimbi la wizi wa vibao hivyo katika mtaa wake, na kwamba tayari vibao sita vimeng’olewa.

 

error: Content is protected !!