Rita Dominic aolewa na Kigogo

HomeBurudani

Rita Dominic aolewa na Kigogo

Muigizaji maarufu kutoka nchini Nigeria, Rita Dominic amepokea pongezi nyingi kutoka kwa mashabiki zake kwa kuweza kufungua ndoa na mume wake wa muda mrefu ambaye ni mjumbe wa Bodi ya Folio Group, mmiliki wa  Daily Times na mashindano ya urembo ya Miss Nigeria pageant.  .

Sherehe hiyo ya harusi ilihudhuriwa na watu maarufu mbalimbali wakiwemo waigizaji wenzake kama Ini Edo, Uche Jombo, Joke Silva, Chioma na Kate Henshawa.

Picha zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zilimuonyesha Rita akiwa amevalia mavazi ya kitamaduni ya Kiigbo huku akicheza kwa furaha katika siku yake hiyo.

Dominic, 46, ni mkongwe wa tasnia ya filamu nchini Nigeria na ameigiza katika filamu nyingi maarufu.

 

error: Content is protected !!