Siri 5 unazopaswa kufahamu kuhusu bahati nasibu

HomeElimu

Siri 5 unazopaswa kufahamu kuhusu bahati nasibu

Ni muhimu kabla hujaamua kuwekeza nguvu zako zote kwenye michezo ya bahati nasibu ukiamini michezo hiyo itakufanya uwe tajiri uyafahamu mambo haya kwa uchache.

1. Bahati nasibu sio suluhisho sahihi la kifedha
Mara nyingi watu wanaamini kupitia bahati nasibu wanaweza kufanikiwa kimaisha, ila mchezo wa bahati nasibu sio mchezo wa uhakika na mara nyingi watu wakipata pesa huzitumia vibaya kwani wanakua hawajajipanga. Ili uweze kuwa na matumizi mazuri ya hela lazima uwe na mipango sahihi ya fedha kabla haujaipata.

2. Bahati nasibu ni biashara
Kwenye biashara yoyote lazima kuwe na faida kwa anayefanya biashara. Hivyo kampuni za bahati nasibu haziwezi kufanya kazi bila kupata faida, na faida hizo zinatokana na hela awekayo mchezaji. Faida inayozotengenezwa na kampuni hizo ni kubwa kiasi kwamba hawaoni shida kutoa sehemu ndogo ya faida hizo kama zawadi kwa wanaocheza mchezo huo.

3. Hakuna mfumo sahihi unaoeleweka
Bahati nasibu nyingi hazina mfumo sahihi wala uwazi wa vipi mshindi anapatikana, michezo hiyo huchezeshwa na kompyuta ili kupata mshindi hivyo inaweza kukuchukua muda kushinda ni bora kutumia kiasi hicho cha pesa kuwekeza kwenye biashara.

4. Hukuathiri kisaikolojia
Kampuni za kubahatisha hutumia mbinu na maneno ya kukufanya uhisi kuwa ni wewe ambaye unakaribia kushinda, unaweza kukuta anacheza sana na kushinda hela ndogo au wanakwambia mshindi anaekuja ni wewe usiache kucheza au cheza zaidi ili ushinde. Kutokana na hali hiyo mchezaji hutaman kuendelea kucheza zaidi. Hali hii inaweza kukufanya ukawa na msongo wa mawazo pale utakapokua unacheza mara nyingi alafu haushindi.

5. Utasahau kuhusu malengo yako
Watu wanaocheza bahati nasibu wanaamini katika kushinda tu na mfumo mzima wa maisha yao hubadilika na kuamini siku atakayoshinda bahati nasibu ndio siku ambao amefikia malengo yake. Wengi husikika wakisema nitatoka tu, mimi huu mchezo utanitoa tu, anasahau majukumu mengine ambayo yana mahitaji na akili yake inahamia kwenye bahati nasibu.

error: Content is protected !!