Burna Boy ataka bangi iruhusiwe Nigeria

HomeBurudani

Burna Boy ataka bangi iruhusiwe Nigeria

Nyota wa muziki kutoka nchini Nigeria, Damini Ebunoluwa Ogulu maarufu kama Burna Boy amesema kwamba ni vyema sheria ikaruhusu matumizi ya bangi nchini humo kwani haina madhara kama ambavyo wengi wanasema.

Akihojiwa kwenye kipindi cha ‘Home Grown Radio’ jijini Los Angeles, Burna alieleza kwamba watu wengi wanatumia bangi lakini hawataki kutangaza hadharini lakini hamna madhara mabaya yoyote iwapo ukitumia.

“Kila mtu anatumia bangi lakini hakuna anayetaka kusema au kukutwa nayo.” amesema Burna Boy.

Pia amesema watu wazima na viongozi wamefanikiwa kutoa elimu ya kwamba endapo mtu atatumia bangi basi atakuwa chizi jambo ambalo yeye amekataa na kusema ni uongo hivyo bora sheria iruhusu matumizi ya bangi.

error: Content is protected !!