Wasanii wa Bongo mjifunze kwa Wizkid

HomeBurudani

Wasanii wa Bongo mjifunze kwa Wizkid

Mwaka 2021 umekuwa ni wa baraka sana kwa nyota kutoka nchini Nigeria Wizkid kwani ngoma yake ya ‘ Essence’ imekuwa ikipasua miamba ya dunia kwa kusikilizwa mara nyingi hivyo kumfanya msanii huyu kupata mafanikio makubwa.

Mafanikio hayo ni pamoja na kufanya Remix na Justin Bieber pamoja na kuburudisha mashabiki zake kwa siku tatu yani tarehe 28 mwezi Novemba, 29 na Desemba 1 kwenye uwanja mkubwa wa O2 Arena Jijini London, Uingereza.

Katika siku zote hizo Wizkid hakuwa anaimba pekee yake licha ya kwamba tamasha hilo lilimuhusu yeye na albam yake ya ‘Made in Lagos’, aliweza kuwapandisha jukwaani wasanii wakubwa kwa wadogo na kuwapa nafasi ya kuimba nao jambo lililoongeza furaha kwa mashabiki waliokuwepo.

https://clickhabari.com/wizkid-amnyoosha-tena-diamond-platnumz/

Siku ya kwanza Wizkid alimpandisha jukwaani mkali wa muziki kutoka Marekani, Chris Brown na kuimba jambo lilioibua hisia za mashabiki wengi kwani Brown alizuiwa kusafiri kwenda U.K. baada ya kukiri kosa la kumpiga mpenzi wake wa wakati huo Rihanna mwaka wa 2009.

Wizkid hakuishia hapo tu aliwapandisha wasanii kutoka Nigeria kama Burna Boy, Tems, Ckay, Koffee, Bella Shmurda, Buju, Giggs, Skepta, Tems, Lojay, BlaqBonez, Tay Iwar, huku akiwaomba mashabiki zake wawaunge mkono wasanii hao kama jinsi wanavyomuunga yeye.

Kitendo cha Wizkid kupandisha wasanii wenzake bila kujali ukubwa wao, udogo wala lebo wanazotokea kinajenga muungano katika ya wasanii ndani ya Nigeria na ndio chanzo cha mziki wao kusikilizwa na kupendwa sana nje ya Afrika, hivyo basi wasanii wa Tanzania ni wakati wenu sasa kuungana ilikuweza kufika mbali zaidi, Jifunzeni kupitia Wizkid, Davido na Burna Boy.

error: Content is protected !!