Wizkid amnyoosha tena Diamond Platnumz

HomeKimataifa

Wizkid amnyoosha tena Diamond Platnumz

Nyota wa muziki kutokea nchini Nigeria, Wizkid ‘#BigWiz’ ameshinda tuzo tatu(3) za AFRIMA 2021 zilizotolewa usiku wa kuamkia leo Nov. 22 2021 katika vipengele mbalimbali huku akiwapiga chini wasanii wengine kama Diamond Platnumz, Davido, MHD, Fally Ipupa, Focalistic, Omah Lay, na Burna Boy.

Wizkid amechukua tuzo hizo kupitia vipengele vya msanii bora wa mwaka akichuana na Diamond Platnumz, Davido pamoja na Burna Boy, wimbo bora wa mwaka ‘Essence’ na kolabo bora la mwaka akiwa na msanii wa kike Tems.

Mwaka 2021 umekua wa neema kwa Wizkid kwakuweza kung’ara duniani kupitia wimbo wake wa Essence mpaka kuwavutia watu wengi kama Justin Bieber aliyefanya nae remix, na mkongwe wa muziki kutoka nchini Marekani Neyo aliyeweka wazi kwamba anatamani angeiandika yeye nyimbo hiyo huku akisema hatua kubwa aliyoifikia Wizkid na anajivunia katika hilo na pia ni mmoja kati ya mastaa wa kizazi hiki kipya anaowapa heshima yake.

error: Content is protected !!