Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 15 (Lingard kuachana na Man United mwezi January, huku Klabu ya Liverpool ikimnyatia Raphinha)

HomeMichezo

Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 15 (Lingard kuachana na Man United mwezi January, huku Klabu ya Liverpool ikimnyatia Raphinha)

Beki wa Chelsea Cesar Azpilicueta 32, na mchezaji mwenzake Andreas Christensen 25, ni miongoni mwa wachezaji ambao wanafuatiliwa na klabu ya Barcelona kwa usajili msimu ujao (Fichajes – Spanish).

Real Madrid, Newcastle United, Arsenal na Liverpool ni miongoni mwa klabu ambazo mshambuliaji Raheem Sterling 26, anaweza kujiunga nazo baada ya kutangaza kuwa yuko tayari kuondoka Manchester City (Express).

Kiungo wa kati wa Manchester United Jesse Lingard (28) yupo tayari kuondoka klabu hiyo mwezi Januari ili kuimarisha nafasi yake ya kuteuliwa katika kikosi cha England cha Kombe la Dunia mwaka ujao. Klabu za Barcelona na AC Milan zinahusishwa na usajili wa mchezaji huyo (Mirror).

Leeds United inamfuatilia Beki wa Ajax Noussair Mazraoui 23, ambaye pia amehusishwa na uhamisho wa Arsenal na Roma (Football Insider).

> Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 14 (Phoden agomea mkataba mpya, huku Rabiot njia nyeupe kujiunga Newcastle)

Klabu ya Arsenal haina mpango wa kumuachilia mshambuliaji wake Gabriel Martinelli 20, kuondoka kwa mkopo dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa mwezi Januari (90min).

Rais wa Lille Olivier Letang amefichua siri kuwa kiungo wa kati wa Portugal Renato Sanches 24, ataruhusiwa kuondoka klabu hiyo ikiwa klabu kubwa itawasilisha ofa ya kumnunua dirisha dogo la usajili mwezi Januari mwakani (Express).

Klabu ya Tottenham imeonyesha nia ya kuhitaji huduma ya beki wa Stoke City Harry Souttar, huku Aston Villa ikiwa tayari inamnyatia kiungo huyo wa Aaustralia (Football Insider).

Klabu ya Fenerbahce inaangalia uwezekano wa kumnunua kiungo wa kati wa Tottenham na England Ryan Sessegnon 21, dirisha la usajili litakapofunguliwa mwezi Januari (Sun).

Newcastle United wamewasiliana na wakala wa kiungo wa kati wa Real Betis Nabil Fekir, 28 (Footmercato – French).

Liverpool wameonesha nia ya kutaka kumsajili winga wa Leeds United Raphinha 24, dirisha la usajili litakapofunguliwa mwisho wa msimu huu, wakala wa mchezaji huyo amedokeza (Globo Esporte – Portuguese).

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta ana orodha ya wachezaji anaopania kuwasajili, wachezaji hao ni pamoja na Tariq Lamptey 21, wa Brighton, James Justin 23, wa Leicester City, na Max Aarons 21, wa Norwich. (Fichajes – Spanish).

error: Content is protected !!