Waziri Kikwete: Utumishi wa umma ni kujibu kero za wananchi

HomeKitaifa

Waziri Kikwete: Utumishi wa umma ni kujibu kero za wananchi

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema serikali imedhamiria kuwa na utumishi wa umma unaojibu changamoto zinazowakabili wananchi wake.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufafanuzi wa hatua mbalimbali za utekelezaji wa zoezi hilo, Waziri Kikwete amesema Serikali inapanga utumishi wa umma ili uweze kuleta tija.

“Serikali inataka kuupanga utumishi wa umma ili uweze kuleta tija kama ambavyo Mhe. Rais alieleza Dkt. Samia Suluhu wakati akihutubia bunge kwamba anataka utumishi wa umma ambao unakwenda kujibu kero za wananchi, utumishi wa umma ambao unakwenda kutoa majawabu ya shida za wananchi” amesema Waziri Kikwete.

Aidha, Waziri Kikwete amesema katika kufikia malengo hayo, Serikali ipo katika hatua za mwisho za kusambaza mifumo itakayosimamia na kuratibu utendaji wa utumishi wa umma nchini.

error: Content is protected !!