Gloria apangiwa shule ya wavulana kujiunga kidato cha kwanza

HomeKimataifa

Gloria apangiwa shule ya wavulana kujiunga kidato cha kwanza

Gloria Adhiambo Owino mwenye umri wa miaka 14 kutoka nchini Kenya amejikuta akipangiwa kujiunga kidato cha kwanza katika Shule ya Wavulana na Lenana ambapo awali yeye na familia yake walifurahia kwa kuwa matokeo yalionyesha amepata alama za juu.

Confusion as female student in Siaya gets Form One placement in a boys' national school

Furaha hiyo ilipotea baada ya Gloria kwenda kuchuka barua yake ya wito na kugundua kwamba alikuwa amepangiwa kujiunga na shule ya wavulana.

Mwanafunzi huyo ambaye sasa amebaki bila msaada amesema amekaa kusubiri barua nyingine lakini hakupata jambo linaloweza kumfanya akashindwa kuendelea na masomo kwani familia yake ni duni haiwezi kumlipa ada ya kwenda shule binafsi.

Gloria ambaye anatamani kwenda Shule ya Wasichana Kisumu lakini wazazi wake hawawezi kumudu gharama za shule hiyo, ameiomba Serikali na wadau wengine waweze kumsaidia.

Ndoto ya Gloria ni kuja kuwa daktari wa tiba hapo baadae.

 

error: Content is protected !!