Mpoto afunguka kuhusu ugawaji wa Mirabaha kwa wasanii

HomeBurudani

Mpoto afunguka kuhusu ugawaji wa Mirabaha kwa wasanii

Baada ya tukio la Uzinduzi wa Tuzo za Muziki Tanzania 2022 na ugawaji wa pesa za mirabaha zinazotokana na kazi za Wasanii zinazotumika kwenye maeneo mbalimbali kama kwenye Redio na Televisheni, Mshairi nguli kutoka nchini Tanzania Mrisho Mpoto maarufu kwa jina la ‘Mjomba’ amefunguka na kusema yale aliyojifunza kutokana na tukio hilo lililofanyika kwenye Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mpoto aliorodhesha mambo makuu 7 ambayo amejifunza na kuyachukua wakati wa tukio hilo.

“Tuzo zikianza kila mmoja apeleke kazi yake, Tusiwe na matokeo yetu mkononi, Maamuzi yatatolewa kwa kazi iliyotumwa, Tusiwatafute majaji kwa ajili ya rushwa, Utakaepangwa nae ni mshindani mwenzio usimdharau hata kidogo, Hizi ni tuzo zetu tunatakiwa kuzipenda na kuzilinda zisife tena na Kielewe vizuri unachoshindania”, ameandika Mrisho Mpoto.

Mpoto alia na waimba “amapiano” Tanzania

Katika ugawaji wa mirabaha, Kwaya ya Mtakatifu Cecilia ya Arusha waliongoza kwa kupata pesa Milioni 8.7, namba 2 akiwa muimbaji Alikiba aliyepata Milioni 7.5, Rose Muhando alipata Milioni 5.7 na wengine ni Christina Shusho, Ibraah, Maua Sama, Nandy, AY na Saraphina.

error: Content is protected !!