Tanzania ya pili uzalishaji wa tumbaku Afrika

HomeKimataifa

Tanzania ya pili uzalishaji wa tumbaku Afrika

Waziri wa Kilimo nchini Tanzania, Mhe. Hussein Bashe amesema takwimu za hivi karibu zinaonyesha Tanzania imekuwa mzalishaji wa pili mkubwa wa tumbaku barani Afrika.

Waziri Bashe amesema uzalishaji wa tumbaku umeongezeka kutoka tani 50,000 hadi tani 122,858 msimu wa 2023/2023 ikiwa ni ongezeko kubwa katika kipindi cha mwaka mmoja tu.

Mpaka mwezi Desema 2023, thamani ya mauzo ya tumbaku kutoka Tanzania ilifika dola milioni 316 na utabiri unaonyesha kuwa inaweza kuongezeka hadi dola milioni 400 mwishoni mwa msimu. Ongezeko hili linathibitisha athari chanya ya sekta ya kilimo kwenye ukuaji wa uchumi wa jumla wa Tanzania.

Ikilinganishwa na takwimu za uzalishaji wa tumbaku za hivi karibuni kwa msimu wa 2022/23 barani Afrika, nafasi mpya ya Tanzania ni muhimu:

Zimbabwe: Tani 296,000.
Tanzania: Tani 122,858.
Malawi: Tani 121,000.
Msumbiji: Tani 65,800.
Zambia: Tani 44,000.
Uganda: Tani 13,000.

Nchi nyingine, ikiwa ni pamoja na Afrika Kusini na Cameroon, zilizalisha chini ya tani 20,000 kila moja.

error: Content is protected !!