Kenya yaomba msaada wa dawa za TB Tanzania

HomeKimataifa

Kenya yaomba msaada wa dawa za TB Tanzania

Waziri wa Afya wa Kenya Susan Nakhumicha Wafula amesema kutokana na uhaba wa dawa za kutibu kifua kikuu au TB, Serikali yao ilichukua uamuzi wa kuomba msaada kutoka Tanzania.

Waziri Wafula alisema mwisho wa mwezi wa Septemba na Oktoba mwaka jana, Kenya ilikua na uhaba wa dawa hizo lakini iliomba msaada na baada ya kupata iliweza kuzigawa katika hospitali zake.

“Mwishoni mwa mwezi Septemba na Oktoba mwaka jana tulikuwa na uhaba wa dawa za kutibu kifua kikuu au TB lakini tulichukua uamuzi wa kuomba msaada kwa jirani zetu Tanzania na tulipewa. Tuliweza kupata dawa za kutosha na kuzisambaza.” amesema Waziri Wafula.

Aidha, Waziri Wafula amesema serikali ya Kenya sasa inahakikisha ina akiba ya kutosha ya dawa hizo ili wagonjwa waweze kuzipata kwa wakati.

 

error: Content is protected !!