Ronaldo afiwa na mtoto

HomeUncategorized

Ronaldo afiwa na mtoto

Bingwa wa dunia wa mpira wa miguu na mchezaji wa timu ya Manchester United, Christiano Ronaldo ‘CR7’ na mpenzi wake Georgina Rodriguez wamepoteza mtoto wao wa kiume usiku wa kuamkia leo.

Kwa miezi kadhaa sasa, tangu Oktoba 2021, wawili hao wamekuwa wakituma picha zenye kuonesha kuwa wanatarajia kupata mapacha wakike na kiume huku akiandika katika moja ya picha hizo kuwa;

“Ninafurahi kutangaza kuwa tunatarajia mapacha. Mioyo yetu imejaa upendo – hatuwezi kungoja kukutana nanyi,” aliandika Ronaldo.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Cristiano Ronaldo (@cristiano)

Krismasi walirusha mtandaoni video nyingine yenye kujuza jinsia za mapacha hao.

Usiku wa jana wawili hao kupitia mtandao wa Instagram wametoa tamko kuhusu kifo cha pacha wa kiume aliyefariki muda mfupi baada ya Georgina kujifungua.

Aidha wameweka bayana kuwa ni kipindi kigumu cha huzuni sana kwao lakini bado wana sababu ya kutokata tamaa.

“Kuzaliwa tu kwa mtoto wetu wa kike kunatupa nguvu ya kuishi katika kipindi hiki, tukiwa na matumaini na furaha,” limesema tangazo hilo.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Cristiano Ronaldo (@cristiano)

Kwa sasa Ronaldo ana jumla ya watoto watano wawili, akiwemo pacha wa kike na mpenzi wake Georgina.

error: Content is protected !!