Morocco yaandika historia

HomeKimataifa

Morocco yaandika historia

Timu ya Taifa ya Morocco imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la dunia inayoendelea huko nchini Qatar baada ya kuifunga timu ya Taifa ya Ureno kwa goli moja kwa bila.

Ushindi huo wa bao moja lililofungwa naye En- Neysir katika dakika ya arobaini na mbili (42) Lilitosha kuipeleka Morocco katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo mikubwa kabisa ya soka duniani.

Morocco ambayo ndio timu ya kwanza ya Afrika kuwahi kufuzu hatua ya robo fainali imeandika Historia mpya kwa kuwa timu ya kwanza kutoka Afrika kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ya dunia.

error: Content is protected !!