Atengwa baada ya kuimba na Harmonize

HomeBurudani

Atengwa baada ya kuimba na Harmonize

Muimbaji wa nyimbo za injili Jane Misso ambaye hivi karibuni ametoa wimbo akiwa na msanii wa bongo fleva, Rajabu Abduli Kahali maarufu kama Harmonize amesema wapo baadhi ya watu waliomtenga baada yakumshirikisha mmiliki huyo wa lebo ya Konde Gang kwenye wimbo wa Omoyo.

“Tunatofautiana sana uwelewa na sio makanisa yote yatakutenga, kuna wengine mbona wame-support , maaskofu wengi, wachungaji wengi wamefurahia sana wamefurahi mno, kitu ambacho sikutegemea lakini wengine wameonekana kukwazika na hata kuna wengine nilikua na safari zangu kuelekea sehemu fulani wamesema wame-cancel lakini mimi sishangai,” alisema Jane Misso.

Pia ameeleza kwamba anawapa muda watu wanaohoji kwanini ameamua kuimba na Harmonize kwa kusema hata Yesu alijichanganya na wadhambi hivyo hajaona kama kuna tatizo. 

Aidha, Jane Misso amemwagia sifa Harmonize kwa kusema kuwa ni kijana muelewa, mnyenyekevu na mwenye heshima na ndio maana hakusita kufanya naye kazi kwani alijua nia yake ni nzuri.

error: Content is protected !!