Mrithi wa Panya Magawa ni Kennedy

HomeKitaifa

Mrithi wa Panya Magawa ni Kennedy

Baada ya Panya Magawa kufariki dunia mwanzoni mwa mwaka huu , Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), mkoani Morogoro, kimempata mrithi wake mwenye jina la Kennedy ambaye ataendeleza majukumu aliyokuwa akifanya Magawa.

Hayo yalisemwa jana na Msaidizi wa utafiti Kitengo cha Apopo, SUA, Dk. Said Mshana kuwa Kennedy anafanya vizuri kazi na ameongezewa majukumu. 

“Kwa kifupi panya Kennedy anaendelea vizuri na majukumu yake ya kila siku ambapo tumemuongezea majukumu zaidi ikiwamo utafutaji wa binadamu wakati wa majanga jambo ambalo litaleta tija sana kwa taifa letu,” alisema Mshana.

Alisema zoezi la utafutaji binadamu wakati wa majanga mafunzo kwa panya huyo linaendelea kwa kufungiwa kamera mgongoni ambayo itakuwa ikionesha matukio yote yanayoendelea ikiwa ni pamoja na kunasa sauti za waathirika wa tukio.

Pia, amesema Kennedy amebobea kusaidia watu kwenye majanga hasa nyumba zilizobomoka kwa kubeba kamera kama binadamu kisha kurekodi matukio.

Aidha, alisema panya huyo amefundishwa kugundua vimelea vya kifua kikuu na kutegua mabomu ardhini na kwamba wapo waliotumwa nje ya nchi kama Zimbabwe, Msumbiji na Kambodia kwa ajili ya kutegua mabomu ardhini kutokana na nchi hizo kuathiriwa zaidi ili ardhi itumike kwa kilimo. 

error: Content is protected !!