Rais Samia ataka Kituo cha Watoto kujengwa Soko la Njombe

HomeKitaifa

Rais Samia ataka Kituo cha Watoto kujengwa Soko la Njombe

Uongozi wa Mkoa wa Njombe umetakiwa kuweka kituo maalumu cha kulelea watoto katika soko kuu la Njombe kwa ajili ya watoto wa wanawake wanaofanya biashara kwenye soko hilo.

Agizo hilo limetolewa jana Agosti 10, 2022 na Rais Samia Suluhu, wakati akizindua soko hilo la kisasa.

“Nimepita hapa nimeona wanawake wengi wana watoto wadogo, wapo wanaowabeba mgongoni, wengine wanacheza chini mama zao wanaendelea na biashara.” Amesema Rais Samia na kuongeza

“Ninachoona kuna haja ya kuwa na eneo maalum ambalo litawekwa kituo cha kulelea watoto ili kuwapa nafasi wazazi wao kuendelea na biashara,” amesema.

Hata hivyo, Rais Samia amewataka wanawake watakaokitumia kituo hicho kuwa tayari kuchangia huduma za kuwatunza watoto hao.

error: Content is protected !!