Wananchi wa Newala wampa Rais Samia maua yake

HomeKitaifa

Wananchi wa Newala wampa Rais Samia maua yake

Baadhi ya wafanyabiashara wa Wilaya ya Newala wamepongeza na kumshukuru Mhe: Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kufungua mipaka ya kuingia na kutoka nchi jitani ya Msumbiji.

Wakizungumza na chombo cha habari cha MTWARA DIGITAL NEWS 24 Bwn: Issa Lali na Iddy Kayanda wamesema uamuzi wa kufungua mpaka wa Tanzania na Msumbiji kupitia Newala,ni uamuzi sahihi kwasababu itarejesha uimara wa uchumi kwa wafanyabiashara kutokana na muingiliano wa watu kutoka upande wa Msumbiji kwasababu watu wengi wa upande wa kaskazini mwa Msumbiji hutegemea kununua bidhaa zao nchini Tanzania hasa katika mji wa Newala.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Newala Mhe: Rajabu Kundya amesema wao kama serikali ya Wilaya tayari wameweka mazingira mazuri kwa wafanyabiashara hao kwaajili ya kutumia mpaka huo kwenye shughuli zao na anaamini kunguliwa kwa mpaka huo kunaenda kuongeza pato kwa wafanyabiashara na Wilaya kwa ujumla.

 

error: Content is protected !!