Rais Samia ang’ara tena kimataifa

HomeKimataifa

Rais Samia ang’ara tena kimataifa

Kwa mujibu wa jarida la TIME 100, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu ametajwa katika orodha ya viongozi 100 wenye ushawishi mkubwa duniani. 

Rais Samia ametajwa katika orodha hii kutokana na uongozi wake wa kusisimua tangu alipoingia madarakani Machi 19, 2021 na kuleta mabadiliko makubwa kwa nchi ya Tanzania ikiwemo kufungua mlango wa mazungumzo kati ya wapinzani wa kisiasa, hatua zimechukuliwa ili kujenga upya imani katika mfumo wa kidemokrasia, juhudi za kuongeza uhuru wa vyombo vya habari na amekuwa mfano wa kuigwa na wanawake na wasichana wengi.

Mnamo Septemba 2021, miezi michache ya urais wake, Suluhu Hassan alitoa hotuba ya kihistoria kama kiongozi mwanamke wa tano pekee wa Kiafrika aliyewahi kuhutubia mkutano mkuu wa Baraza la Umoja wa Mataifa.

“Kama Rais wa kwanza mwanamke katika historia ya nchi yangu,” alisema, “mzigo wa matarajio ya kuleta usawa wa kijinsia ni mzito zaidi kwenye mabega yangu.”

Rais Samia ameungana na marais kutoka nchi nyingine katika orodha hiyo wakiwemo Volodymir Zelenskyy wa Ukraine, Xi Jinping wa China, Vladimir Putini wa Urusi na Joe Biden wa Marekani.

 

error: Content is protected !!