Mwanafunzi ajeruhiwa kisa Mahusiano

HomeKitaifa

Mwanafunzi ajeruhiwa kisa Mahusiano

Mwanafunzi wa kike wa kidato cha tatu katika shule ya Sekondari Mbogi, Wilayani Tarime amejeruhiwa vibaya kwa kisu na kuachwa na majeraha makubwa.

Kijana aliyemjeruhi mwanafunzi huyo, huku chanzo cha tukio hilo kikielezwa kuwa ni kulazimisha uhusiano na binti huyo.Mashuhuda wa tukio hilo walisema mwanafunzi huyo alipiga kelele za kuomba msaada , lakini hadi wanafika alishajeruhiwa na mhusika kukimbia kusikojulikana.

Kijana aliyefanya tukio hilo, alimsubiri mwanafunzi huyo akiwa anatoka kuteka maji, ndipo akafanya uhalifu huo.

Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Afya anakopatiwa matibabu, Dkt Stephen Mtimba alisema msichana huyo alijeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili kwa kitu chenye ncha kali na kwamba anaendelea na matibabu huku afya yake ikiimarika.

Binamu wa mwanafunzi huyo amesema, binamu yake alikua akilalamika kwa ndugu zake  mara kadhaa kuhusu kunyanyaswa kijinsia na kijana huyo kiasi cha kusababisha taarifa hizo kuripotiwa katika uongozi wa kijiji wiki mbili zilizopita.

error: Content is protected !!