P Square waungana tena rasmi

HomeBurudani

P Square waungana tena rasmi

Mapacha waliokuwa wakiunda kundi la P square, Peter na Paul wamepatana rasmi baada ya kupitia vita vikali kati yao kwa miaka kadhaa na kusababisha kusambaratika kwa kundi lao mwaka 2016.

Hivi karibuni walionyesha dalili za kupatana baada ya Paul kuonekana akitoka na watoto wa kaka Peter na kwenda nao kwenye matembezi, pia wawili hao walianza kufuatana kwenye mtandao wa instagram hivyo kuwaacha wengi na maswali kama mapacha hao wamesameheana au bado.

> Dalili kwamba P Square wamerudiana

Baada ya miaka mitano ya kutokuwa na maelewano , rasmi mapacha hao wameweka tofauti zao pembeni na usiku wa jana wameonekana wakisalimiana na kukumbatiana, pia kila mmoja akimpost mwenzake kumtakia heri ya siku ya kuzaliwa kwani mapacha hao husherekea siku yao ya kuzaliwa tarehe 18, Novemba kila mwaka.

Mashabiki wa mapacha hao wamefurahishwa na maamuzi hayo kwani ni muda mrefu tangu watoe ngoma pamoja.P Square ni kundi liliofanya  vizuri Afrika na duniani kwa ujumla kupitia nyimbo zao kama Do Me, Temptation, Personally na nyingine nyingi.

error: Content is protected !!