Dalili kwamba P square wamerudiana

HomeBurudani

Dalili kwamba P square wamerudiana

Wasanii wakubwa mapacha kutoka nchini Nigeria waliokuwa wanaunda kundi la P Square ambalo lilipata umaarufu zaidi duniani kupitia nyimbo zao kadhaa kama Do me, Personally, Temptation na nyingine nyingi wameonyesha dalili yakuweka tofauti zao pembeni tangu watengane mwaka 2016.

Dalili mojawapo ni video iliyowekwa kwenye ukurasa wa Instagram wa mke wa Paul, Anita ikimuonyesha Peter akiwa na watoto wa Paul alipowapeleka matembezini na kuwanunulia zawadi kama cheni za thamani na midoli mbalimbali nchini Marekani.

Pia kila mtu amem-follow mwenzake kwenye mtandao wa Instagram kwani baada ya wawili hao kutengana kila mmoja aliacha kumfuatilia mwenzake kwenye mitandao ya kijamii na dalili nyingine ni kaka yao mkubwa , Jude Okoye kuanza kum-follow tena Peter kwenye ukurasa wake wa Instagram kwani baada ya kundi hilo kuvunjika Jude alionekana akichagua kuwa upande wa Paul.

Baada ya wawili hao kutengana Peter alianza kutumia jina la Mr. P huku Paul akitumia Rudeboy.
Hata hivyo bado haijafahamika rasmi kama kweli kufanya kazi pamoja au wameamua tu kusameheana huku kila mtu akiendelea kufanya kazi zake mwenyewe.

error: Content is protected !!