Rais Samia atimiza ahadi reli ya SGR

HomeKitaifa

Rais Samia atimiza ahadi reli ya SGR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameshuhudia utiaji saini Mkataba wa ujenzi wa reli ya kisasa kwa kipande cha nne kutoka Tabora hadi Isaka.

Hafla ya utiaji saini iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam imehusisha mikataba miwili,mmoja ukiwa ni kati ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) NA Yapi Merkez ya Uturuki.

Mkataba mwingine ni kati ya TRC na Kampuni ya KORAIL ya Korea kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo ya uendeshaji wa reli ambapo ni matayarisho ya kuwajengea watanzania uwezo wa kuiendesha na kuisimamia wenyewe.

Vile vile, Rais Samia amesema ujenzi wa kipande cha reli hii chenye kilomita 165 utasaidia kuunganisha mikoa tisa ya Dar es Salaam, Pwani,Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora, Simiyu, Shinyanga na Mwanza.

Kwa upande mwingine ujenzi huu pia utaiunganisha Tanzania na nchi za Uganda, Burundi, Rwanda,DRC, na Sudan Kusini na kuifanya kuwa kitovu cha biashara.

Gharama za ujenzi wa kipande cha nne katika Mkataba huu ni shilingi Trilioni 2.092 na gharama za vipande vyote vitano kutoka Dar es Salaamhadi Mwanza ni shilingi Trilioni 16.792.

error: Content is protected !!