Wananchi Ngorongoro wakubali kuhama

HomeKitaifa

Wananchi Ngorongoro wakubali kuhama

Wananchi wanaoishi ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) wamesema kupata haki miliki ya nyumba ndani ya mamlaka hiyo ni ndoto hivyo ni vema kuhamia eneo la Msomera wilayani Handeni mkoani Tanga ili waweze kupata hati miliki wanayoweza kuitumia kukopeshwa katika taasisi za fedha.

Wananchi hao pia wameomba kujengewa kituo cha polisi sambamba na huduma muhimu za kijamii ili wanapohama waweze kujisikia wapo mahali tulivu penye kuhitaji kujikwamua kiuchumi kutokana na fursa zilizopo eneo husika.

Lobikoki Mollel ni kati ya wananchi waliokuwa wakiishi Ngorongoro, alisema hawakuwahi kupata hati miliki hivyo wanaomba serikali iwahamishe.

“Hatimiliki ina heshima yake, tunaomba serikali ituondoe huku haraka twende zetu Msomera tukafungue macho yetu na kubuni biashara zitakazotuinua kiuchumi,” alisema Mollel.

Aidha, wananchi hao wamesema wameachana na vishawishi vya wachumia tumbo wenye mashirika yasiyo ya kiserikali wanaodanganya wananchi juu ya kuhama kwa hiari.

 

error: Content is protected !!