WAKE: Tuna haki ya kwenda Dubai kama michepuko

HomeKimataifa

WAKE: Tuna haki ya kwenda Dubai kama michepuko

Kikundi cha wanawake jijini Kampala wamefanya maandamano asubuhi hii ya leo tarehe 11 mwezi Aprili wakishinikiza wanaume zao kuwaongezea kiwango cha pesa ya matumizi wanachowaachia asubuhi wakidai gharama za maisha zimepanda na pia wanaume hao hawawapi heshima wanayostahili kutokana na huduma wanazopata kutoka kwa michepuko.

Wakiwa wameshika mabango yenye jumbe mbalimbali kama ‘hata sisi tunastahili kupelekwa Dubai kama michepuko yenu’, wanawake hao wamelaani kitendo cha kuachiwa kiasi kilekile cha fedha walizokuwa wakiachiwa mwaka jana ilhali sasa gharama zipo juu.

Aidha, Polisi nchini Uganda wamesema wanawake hao wamekamatwa na kwa sasa wanashikiliwa kituo cha Polisi Kampala kwa kuwa maandamano yao ni batili na hajayazingatia sheria.

 

error: Content is protected !!