Chanjo za J&J zilizopelekwa Ulaya kurejeshwa Afrika

HomeKimataifa

Chanjo za J&J zilizopelekwa Ulaya kurejeshwa Afrika

Umoja wa Ulaya (EU) unakusudia kurejesha barani Afrika mamilioni ya chanjo ya Johnson & Johnson zilizotengenzwa nchini Afrika Kusini ambazo hupelekwa kwenye nchi za Magharibi.

Ujumbe wa Umoja wa Afrika (AU) umewaambia waandishi wa habari kuwa chanjo zote ambazo zinazalishwa barani Afrika zitabaki na kusambazwa kwenye nchi za Afrika.

“Jambo hili limesahihishwa, na limesahihishwa kwa njia chanya sana,” amesema Strive Masiyiwa kwa niaba ya AU.

Uamuzi huo umefuatia kukosolewa kwa nchi za Magharibi kuchukua chanjo hizo kutoa Afrika, bara ambalo lina wastani mdogo zaidi wa utoaji chanjo dhidi ya UVIKO-19, ambapo hadi sasa ni wakazi wa Afrika waliopata chanjo ni chini ya 3%.

Hivi karibuni Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera akizungumza kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC alisema kwamba kumekuwa na ubaguzi katika utoaji wa chanjo hizo, na kwamba mataifa ya Afrika yanabaguliwa na nchi zilizoendelea ambazo ndizo wazalishaji wakubwa wa chanjo.

error: Content is protected !!