Bei ya mafuta yashuka

HomeKitaifa

Bei ya mafuta yashuka

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa zitakazotumika kuanzia Januari 03, 2024.

Bei ya petroli kwa Mkoa wa Dar es Salaam imeshuka kutoka Sh 3,158 iliyokuwa mwezi Desemba 2023 hadi Sh 3,084 huku dizeli ikishuka hadi Sh 3,078 kutoka Sh 3,226 mwezi Desemba 2023.

Taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo imeeleza kuwa sababu ya kushuka bei za mafuta ni kushuka kwa bei za mafuta katika soko la dunia kwa asilimia 6.03 kwa petroli na asilimia 7.13 kwa dizeli.

Cap-Prices-for-Petroleum-Products-wef-3rd-January-2024-Kiswahili-
error: Content is protected !!