Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini Mtwara kukuza utalii wa matibabu

HomeKitaifa

Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini Mtwara kukuza utalii wa matibabu

Rais Samia Suluhu amezindua Jengo la Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini Mtwara ambayo itakuwa ikitoa huduma za kibingwa na kibobezi.

Hospitali hiyo itahudumia wananchi wa mikoa mitatu ya Lindi, Mtwara na Ruvuma pamoja na nchi za jirani hivyo kuchochea utalii wa matibabu nchini.

Akizungumza wakati wa Ufunguzi huo, Rais Samia aliwasihi watoa huduma kufanya kazi kwa weledi na kuhudumia wananchi ipasavyo.

“Mungu amewateua nyinyi kutoa huduma kwenye jengo hili, niwaombe sana pamoja na changamoto zilizopo Mtwara kazi tunayofanya hapa ni kuokoa maisha ya watu.” amesema Rais Samia.

Aidha katika ufunguzi huo, Rais Samia amekabidhi magari matatu ambapo kati ya gari hizo mbili ni mahususi kwa ajili ya kubeba wagonjwa na gari moja kwa ajili ya kutolea huduma.

 

 

error: Content is protected !!