Bashe: Marufuku kuwauzia madalali parachichi mbichi

HomeKitaifa

Bashe: Marufuku kuwauzia madalali parachichi mbichi

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amepiga marufuku wakulima kuuza parachichi kwa madalali zikiwa hazijakomaa na kuiva.

Bashe ametoa onyo hilo jana Agosti 10, 2022 mkoani Njombe katika ziara ya Rais Samia Suluhusu Hassan.

Akizungumza katika Uwanja wa Sabasaba, Bashe amesema madalali wananunua parachichi zikiwa mbichi, wanaua soko la nje, kwani parachichi hizo zinakuwa hazina ubora.

“Natoa rai kwa wakulima wa parachichi kuacha kuwauzia madalali maparachichi, ambayo hayajakomaa kwani yanaenda kutuulia soko letu la nje, tutakapotoa muongozo viongozi wa mkoa na wilaya msimamie hili vizuri,” amesema.

Amesema Wizara yake imeshatengeneza muongozo ambao utaongoza sekta ndogo ya parachichi, ambao utaongoza msimu unaanza lini, bei za parachichi na ushindani wa soko.

error: Content is protected !!