Sabaya atemwa

HomeKitaifa

Sabaya atemwa

Wakili aliyekuwa akisimamia na kumtetea aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya (35) na wenzake 6 amejitoa katika kesi hiyo huku chanzo kikidaiwa kuwa ni maslahi.

Wakili Fridolini Bwemelo (27) alitangaza uamuzi huo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha mbele ya Hakimu Patricia Kisinda kabla ya kuanza utetezi wa kesi hiyo.

Mmoja wa washtakiwa waliokuwa wakisimamiwa na Wakili Bwemelo, Watson Mwahomange alisema hakuwa na pingamizi kuhusu uamuzi wa wakili wake kujitoa na akasema yuko tayari kujitetea mwenyewe na mahakama iliridhia hilo.

 

error: Content is protected !!