Dakika 34 zamponza Davido

HomeKitaifa

Dakika 34 zamponza Davido

Mwanamuziki maarufu kutokea nchini Nigeria, Davido amelipishwa faini ya Euro 340,000 ambayo inakadiriwa kwa pesa za kitanzania ni zaidi ya Bilioni 1 na Milioni 46. Davido amelipishwa kiasi hiko kama faini baada ya kuzidisha muda wa kutumbuiza katika tamasha lake alilolifanya mwisho wa wiki hii  siku ya jumamosi Machi 5, ndani ya ukumbi wa 02 Arena jijini London, Uingereza.

Tamasha hilo lilitakiwa kuisha majira ya saa tano kamili usiku lakini alizisha muda na tamasha hilo liliisha majira ya saa 5 na dakika 34. Mkali huyo anasema alilijua kabla suala hilo ambapo kwa utaratibu wa ukumbi huo kila dakika moja ambayo inazidi  inatozwa Euro 10,000.

Katika tamasha hilo alilofanya jijini London, Davido alifanikiwa kuuza tiketi zote kabla ya siku ya tamasha  na kufanikiwa kuujaza ukumbi huo, Miongoni mwa wasanii waliomuunga mkono katika tamasha hilo ni mwanamuziki Adekunle Gold ambaye alitumbuiza katika tamasha hilo.

 

 

Newer Post
error: Content is protected !!