Temeke wakamilisha ‘madarasa ya Rais Samia’

HomeKitaifa

Temeke wakamilisha ‘madarasa ya Rais Samia’

Bilioni 3.14 zilizotolewa na serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan zimewezesha kukamilika kwa ujenzi wa vyumba vya madarasa ya sekondari 157 katika wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam ambapo makabidhiano ya vyumba hivyo yalifanyika jana kwenye Shule ya Sekondari Dovya, Chamazi wilayani humo na mgeni rasmi alikua Mkuu wa Wilaya, Jokate Mwegelo.

Jokate alifafanua kwamba vyumba 157 vya madarasa katika shule 25 vimekamilika vikiwa na meza na viti huku akimshukuru Rais Samia Suluhu kwa kuridhia Wilaya ya Temeke kupewa Sh bilioni 3.14 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa hayo ikiwa ni sehemu ya fedha za mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko-19.

“Tuna deni la kumlipa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha watoto wetu wanafanya vizuri katika masomo yao maana fedha alizotupatia ni zaidi ya shilingi bilioni tatu za ujenzi wa madarasa 157, hivyo tutakuwa tumezitendea haki kwa watoto wetu kufaulu,” alisema Jokate.

Pia Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba kukamilika kwa madarasa hayo kunakwenda kufanya idadi ya wanafunzi ambao watanufaika kuanzia mwaka huu kuwa milioni 12 na kupunguza msongamano wa wanafunzi madarasani.

error: Content is protected !!