Maoni ya ACT Wazalendo kuhusu utendaji kazi wa Kampuni binafsi ya kimataifa ya kuhudumia Makontena Tanzania (TICTS).

HomeKitaifa

Maoni ya ACT Wazalendo kuhusu utendaji kazi wa Kampuni binafsi ya kimataifa ya kuhudumia Makontena Tanzania (TICTS).

Baada ya wadau wa sekta za biashara na usafirishaji kuiomba serikali kutoiongezea mkataba mpya kampuni ya TICTS eneo la bandari ya Dar es Salaam kwa kushindwa kufanya kazi zake kwa ufanisi, Chama cha ACT Wazalendo wametoa maoni juu ya utendaji kazi wa kampuni hiyo ya kuhudumia makontena.

ACT Wazalendo wamesema ni kweli TICTS wameenda kinyume na matakwa ya mkataba ambayo ni kuboresha utendaji ili kuongeza mchango wa bnadari kwenye uchumi wa taifa, kupunguza gharama za kuhudumia shehena zinazopita bandari ya Dar es Salaam, kuvutia shehena za ndani na nje kupita kwenye bandarini na kuingiza teknolojia mpya ili kuwezesha wazawa kupata mbinu mpya za usimamizi.

Kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao kifanisi na kusababisha hasara kwenye uchumi wa taifa, ACT Wazalendo wanaungana na wadau wengine katika suala la TICTS kutoongezewa mkataba kwa kuwa ni wazi imeshindwa kukidhi matarajio ya kukodishwa kwake.

Pia, ACT Wazalendo wameitaka serikali kuichambua TICTS na kutathmini utendaji kazi wake ndani ya miaka 20 iliyopita na kuona faida zake na uwezo wa kufikisha malengo mapya yatakayokuwa katika mkataba ujao.

Aidha, ACT Wazalendo wamesema kwa kuwa serikali imetambua kwamba TICTS imesababisha hasara kwa kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi, ni vyema jambo hilo sasa lisimamiwe kwa umuhimu mkubwa ili kuongeza ufanisi.

 

error: Content is protected !!