Ahadi ya Samia kwa Wananchi wa Chato

HomeKitaifa

Ahadi ya Samia kwa Wananchi wa Chato

Rais Samia Suluhu Hassan amewaahidi wananchi wa Chato mkoani Geita kwamba miradi iliyopangwa itakamilishwa ikiwemo kivyuko cha Chato cha ‘Hapa Kazi Tu’ kilichokamilika kwa asilimia 100 na kugharimu Sh bilioni 3.1, ujenzi wa Kiwanja cha Ndege Chato umefikia asilimia 95 na umegharimu Sh milioni 58.9 na stendi ya mabasi imefikia asilimia 90 iliyogharimu Sh bilioni 13.2

“Nataka niwaahidi wana chato kwamba miradi hii itakapokamilika kabisa nitakuja mwenyewe kuifungua kama ambayo angefanya mwenyewe kama angekuwepo,” alisistiza.

“Tumetoka mbali na tunakokwenda nimbali. Haya tunayopanga yatafanikiwa kama tukidumisha amani na mshikamano wetu kama Watanzania,” alisema Rais Samia Suluhu Hassan.

Aidha, Rais Samia alikumbushia hotuba yake ya kwanza baada ya kuapishwa ambayo alisistiza kuwa ataendeleza mema yote yalioachwa na Dk Magufuli na kuleta mema mengine mapya.

error: Content is protected !!