Fahamu kuhusu sare mpya za wahudumu wa ndege Ukraine

HomeKimataifa

Fahamu kuhusu sare mpya za wahudumu wa ndege Ukraine

Shirika binafsi la ndege nchini Ukraine linalojulikana kama ‘SkyUp Airlines’ linatarajia kuwa na sare mpya kwa wahudumu wake ambazo zitakua suti na raba. Wahudumu hao wa ndege watatakiwa kuvaa raba nyeupe badala ya viatu virefu na suti za suruali zenye rangi ya machungwa badala ya sketi za kubana maarufu kama penseli.

Mabadiliko hayo yanatokana na maoni yaliokusanywa na wahudumu hao, pia mabadiliko hayo yameangalia zaidi uhitaji wakati wa dharura kwani ni salama zaidi kwa mhudumu kutoa msaada akiwa amevaa raba na suruali isiyobana.

Kwa upande wa nywele wahudumu hao hawatakiwi kuwa na rasta isipokuwa watatakiwa kubana nywele zao kawaida tu maarufu kama mkia wa farasi.

error: Content is protected !!