Anusurika kufa baada ya kuua

HomeKitaifa

Anusurika kufa baada ya kuua

Mfanyakazi wa kuhudumia mifugo (jina limehifadhiwa) anadaiwa kumuua mfanyakazi mwenzake wa ndani, Dawiya Iddy kisha kunywa sumu kwa lengo kijiua, jaribio hilo ambalo halikufanikiwa lilitokea Alhamisi katika eneo la Maili Moja , Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Pius Lutumo alikiri kuwepo kwa tukio hilo na mtuhumiwa ambaye kwa sasa anapatiwa matibabu chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani(Tumbi).

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mkoani, Shaban Kasamia alisema siku ya tukio alipigiwa simu kujulishwa hali hiyo na alipofika alikuta tukio limeshafanyika.

Hata hivyo, mwajiri wa wafanyakazi hao ambaye hakutaka kutaja jina lake, alipoulizwa kuhusiana na mauaji hayo hakuwa tayari kuzungumzia tukio hilo.

error: Content is protected !!