Vijana 147 waliojiunga JKT wabainika kuwa na VVU

HomeKitaifa

Vijana 147 waliojiunga JKT wabainika kuwa na VVU

Kamati ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI imesema katika kipindi cha miaka mitatu kilichoanzia 2018, vijana wanaojiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) waliopimwa na kukutwa na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) ni 147.

Ilibainisha hayo jana bungeni ilipowasilishwa taarifa ya utekelezaji wa shughuli zake,taarifa hiyo ilisomwa na mjumbe Yahaya Masare kwa niaba ya mwenyekiti wa kamati.

Masare, Mbunge wa Manyoni Magharibi, alisema JUKT hupokea vijana ambao wamehitimu kidato cha sita ambao huripoti kambini kwa ya mafunzo bili kujali ajili ya afya zao, wote hujumuishwa kuhudhuria mafunzo hayo.

Alisema kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2018 hadi mwaka 2021, JKT ilichukua vijana kwa mujibu wa sheria ambapo mwaka 2019 vijana 20,413; mwaka 2020 vijana 21,282 na mwaka 2021 vijana 25.503. “Hali ya maambukizi kwa vijana waliokuwa kambini kwa mujibu wa sheria kwa miaka hiyo mitatu ni kama ifuatavyo.

“Mwaka 2019 kati ya vijana 20,413 walipimwa, 60 walikutwa na maambukizi; mwaka 2020 kati ya vijana 21,383 waliopimwa, 45 walikutwa na maambukizi na mwaa 2021 kati ya vijana 25,503 waliopimwa, 42 walikutwa na maambukizi,” alibainisha.

Alisema vijana wenye VVU kambini wanapatiwa huduma mbalimbali kama vile ushauri nasaha na kuanzishiwa dawa za kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI (ARV).

 

error: Content is protected !!